Chelsea waipiga chini ofa ya United kwa Mount

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Klabu ya Chelsea imeipiga chini ofa ya klabu ya Manchester United ya euro milioni 40 kwa kiungo wake Mason Mount ikielezwa klabu hiyo imeshikilia msimamo wa euro milioni 80.


Chelsea inataka kumuuza Mason Mount lakini kwa bei ambaye wameiweka wazi ambayo ni euro milioni 80, Lakini klabu ya Manchester United imetoa nusu ofa mpaka sasa lakini baada ya ofa yao kupigwa chini inaelezwa wana mpango wa kurudi na ofa nyingine iliyoboreshwa.


Mpaka sasa kiungo Mason Mount ameshaonesha nia ya kutaka kuondoka na anataka kujiunga na klabu hiyo kutoka jijini Manchester lakini klabu yake imetilia ugumu haswa kwenye suala la bei ambayo inaonekana ni kubwa.


Chelsea inahiaji dau kubwa kwa kiungo Mount lakini inatambua fika kama mchezaji huyo atabaki klabuni hapo pasipo kununuliwa basi anaweza kuondoka bure majira ya joto mwaka 2024 kwani mchezaji huyo amebakiza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya timu hiyo.


Chelsea wako kwenye mchakato wa kutengeneza timu mpya chini ya kocha Mauricio Pochettino na ndio maana wanataka kuuza baadhi ya wachezaji ndani ya timu hiyo haswa kwenye eneo la kiungo na Mason Mount ni miongoni lakini dau limekua changamoto kwa timu hizo.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post