Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Hatma ya Lionel Messi kujulikana masaa machache yajayo, baada ya FC Barcelona kushindwa kufikia makubaliano ya kumsajili hivyo kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na PSG.
FC Barcelona ndio walipewa kipaumbele kumsajili Messi, baada ya kuweka wazi kuwa angependa kurejea katika klabu hiyo. Inaripotiwa kuwa viongozi wa FC Barcelona jana Jumatatu walifanya mazungumzo na Baba mzazi wa Lionel Messi Jorge Messi ambae pia ndio wakala wake.
Lakini Barcelona hawakufikia mahitaji ya Messi kutokana na ukata unao ikabili klabu hiyo. Mahitaji ya Messi kwenye mshahara ni Pauni laki 5 zaidi ya Bilioni 1 na million 472 kwa pesa ya Tanzania.
Inatarajiwa ndani ya wiki hii hatma ya Messi itajulikana atajiunga na timu gani, klabu nyingine zinazomuwania Messi ni Inter Miami ya Ligi Kuu soka Marekani na Al Hilal ya Saudi Arabia.
No comments:
Post a Comment