Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Azam FC imewatupa nje Tanzania Prisons kuwa kuwachapa 3-1, mabao yao yakifungwa na Asharfu Kibeku, George Chande na Abdulkarim Kiswanya, la wapinzani wao likifungwa na Iddy Kichindo.
Mtibwa Sugar imewatoa Coastal Unión kwa kuwachapa 2-0, mabao ya Athumani Makambo na Said Makambo, wakati Kagera Sugar imetupa nje Dodoma Jiji kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Said Said na Kassim Fakhi huku.
Geita Gold ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufungua milango ya Nusu Fainali baada ya kuizaba Mbeya City 2-1. Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Nicodemus Ntarema na Shijja Abdallah, huku la Mbeya City likifungwa na Baraka Mwilubunju.
Nusu Fainali zitapigwa Ijumaa hapo hapo Azam Complex, Geita Gold na Azam FC na Mtibwa Sugar na Kagera Sugar.
No comments:
Post a Comment