Al Ahly wanyakua Ubingwa wa CAF kwa mara ya 11 - EDUSPORTSTZ

Latest

Al Ahly wanyakua Ubingwa wa CAF kwa mara ya 11

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Vigogo wa Afrika, Timu ya Al Ahly wamwfanikiwa kunyakuwa Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu wa mwaka 2022/2023 baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Bingwa mtetezi Wydad Casablanca mchezo katika mchezo wa Fainali ya Mkondo wa pili Jumapili usiku.


Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Mohammed V uliwashuhudia Al Ahly wakijihakikishia Ubingwa kwa bao la dakika za jioni la kusawazisha la mlinzi Mohamed Abdelmonem akisawazisha bao la kuongoza la Wydad lililoffungwa na Attiyat Allah 27’.


Sare ya bao 1-1 ikawafanya Ahly kushinda kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 baada ya kushinda mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Juma lililopita nchini Misri.


Ubingwa huo unawafanya Ahly kuweka rekodi ya kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya 11, mara nyingi zaidi kuliko klabu yoyote.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz