Yanga kutangaza ubingwa mbele ya Dodoma Jiji leo? - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga kutangaza ubingwa mbele ya Dodoma Jiji leo?

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Vinara wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga jioni ya leo watashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi kupepetana na Dodoma Jiji katika mchezo ambao Wananchi wana nafasi ya kutwaa ubingwa kama wataibuka na ushindi


Wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 71, alama nne zaidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili, Yanga inahitaji alama tatu tu kutwaa ubingwa


Simba imesalia na mechi mbili ambazo wakishinda zote watafikisha alama 73, ushindi kwa Yanga leo utawafanya wafikishe alama 74


Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi kwani hata Dodoma Jiji wanahitaji matokeo mazuri ili kujihakikishia usalama wa kubaki ligi kuu msimu huu


Lakini ubora wa kikosi cha kocha Nasreddine Nabi unawapa nafasi zaidi Yanga kushinda mchezo huo na kujihakikishia ubingwa kabla ya kusafiri Afrika Kusini wanakokabiliwa na mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants. Yanga itaondoka nchini Alfajiri ya kesho Jumapili kuelekea Afrika Kusini


Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema shamrashamra kuelekea mchezo huo zitaanza saa sita mchana ambapo kutakuwa na burudani za utangulizi kuelekea muda wa mchezo ambao ni saa 10 jioniDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz