Timu nne zilizo fuzu nusu fainali kombe la shirikisho CAF - EDUSPORTSTZ

Latest

Timu nne zilizo fuzu nusu fainali kombe la shirikisho CAF

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Yanga imeiwakilisha vyema Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika ikiwa moja ya timu nne zilizotinga nusu fainali ya michuano hiyo


Suluhu na bila kufungana dhidi ya Rivers United jana imewavusha Wananchi kwenda nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-0 waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Nigeria


Yanga imeungana na Asec Mimosas iliyopata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya US Monastir pamoja na Malumo Galants ya Afrikca Kusini iliyopata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Pyramids ya Misri


Timu ya nne kutinga nusu fainali ni USM Alger ambayo licha ya kufungwa mabao 3-2 na US FAR ya Morocco, imefuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-4


Katika hatua ya nusu fainali, Yanga itachuana na Malumo Galants wakati Asec Mimosas itachuana na USM Alger


Mechi za nusu fainali zitappigwa May 10 na May 17, Yanga na Asec zikianzia mechi zao nyumbaniDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz