Simba kushusha mashine hii ya ASEC Mimosas - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba kushusha mashine hii ya ASEC Mimosas

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Klabu ya Simba ipo sokoni kuangalia silaha za kuondoa aibu kwa msimu ujao na unyonge wa mashabiki wanaoupitia kwa msimu huu, ikidondosha mataji yote, tayari imetua nchini Ivory Coast ikiwinda winga la ASEC Mimosas, huku mastaa wakilimwa barua.


Winga ambaye Simba ipo naye kwenye mazungumzo mazito kuhakikisha inaipata saini yake kuja kuongeza nguvu zaidi kikosini anatajwa kwa jina la Kramo Aubin.


Huyo jamaa ni hatari kwa mikimbio na Simba ilishaonja joto la jiwe la mchezaji huyo aliwahi kuwafunga mwaka 2022 walipocheza Kombe la Shirikisho la Afrika, wakichapwa mabao 3-0 ugenini lakini pia msimu huu amekuwa bora kwenye michezo yote.


Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kilisema kuwa uongozi upo kwenye hatua nzuri za mazungumzo kwa ajili ya kumalizana na staa huyo wa Asec ambaye wanaamini ataweza kuongeza kitu ndani ya timu.


"Mazungumzo na winga huyo ambaye ni mchezaji tegemeo wa kikosi cha ASEC Mimosas yanakwenda vizuri na kuhusu mchezaji mzawa tumemwambia kocha amfuatilie Shiza Kichuya kwasababu ni winga ambaye anasifa kama alizozitaja.


"Hivyo tunamsikilizia kama mambo yatakwenda kama ilivyopangwa tutaweza kufanya naye mazungumzo," kilisema chanzo hicho.


Chanzo hicho kimesema kuwa wanaendelea na usajili ili kukiandaa kikosi chao mapema kama mapendekezo ya kocha wao alivyotaka kuona wanasajili mapema ili kuingia kambini mapema kujiandaa na msimu mpya.


Kramo Aubin amecheza mechi nane za Kombe la Shirikisho Afrika na kuifungia timu yake mabao manne kwenye michezo hiyo moja alilifunga uwanja wa nyumbani na matatu kwenye michezo ya ugenini.


Staa huyo amecheza timu tatu tu hadi sasa zote zikiwa za nchini kwao Ivory Coast amekuzwa na ASEC Mimosas ambayo alianza kuitumikia mwaka 2015 akicheza kwa misimu miwili baadae akatimkia Africa Sports alicheza msimu mmoja, 2019 alitimkia FC San Penro na 2021 akaamua kurudi tena ASEC Mimosas ambayo anaitumikia hadi sasa.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz