Robertinho aanza na mbadala wa Baleke, Chama Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Robertinho aanza na mbadala wa Baleke, Chama Simba

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kocha Mkuu wa Simba Mbrazili, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amekiangalia kikosi chake na haraka akawaambia mabosi wake, anahitaji mshambuliaji hatari zaidi ya Jean Baleke na kiungo atakayekuwa mbadala wa Clatous Chama.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya timu hiyo, kutolewa na Wydad Casablanca kwa mikwaju wa penalti katika mchezo wa mwisho wa hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa mara baada ya mchezo huo, haraka kocha huyo alifanya kikao na baadhi ya Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, waliosafiri na kikosi hicho.

Ally alisema kuwa anaamini ubora wa wachezaji lakini, maboresho makubwa yanahitaji katika kuelekea usajili wa msimu ujao, ameomba asajiliwe straika mwenye uwezo zaidi ya Baleke.

Alisema kuwa kocha huyo anapata ugumu wa kupata matokeo kimbinu, kutokana na kuwepo mshambuliaji mmoja pekee tishio kwa wapinzani ambaye ni Baleke pekee.

Aliongeza kuwa pia kocha huyo katika kikao hicho ametoa mapendekezo ya kusajiliwa kiungo mshambuliaji mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza mabao kwa wenzake zaidi ya Chama.

“Baada ya mchezo wa marudiano dhidi ya Wydad Casablanca, kocha Robertionho alifanya kikao na viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi tukiwa hotelini Nigeria.

“Kikubwa ni kutoa tathimini ya timu hiyo, katika ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Afrika na katika kikao hicho ametoa mapendekezo ya usajili wa wachezaji wapya.

“Lengo ni kutengeneza timu itakayokuwa bora na tishio katika Ukanda huu wa Afrika na zaidi kufika hatua ya Nusu Fainali hadi Fainali baada ya misimu mitatu kuishia Robo,” alisema Ally.Kocha Mkuu wa Simba Mbrazili, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amekiangalia kikosi chake na haraka akawaambia mabosi wake, anahitaji mshambuliaji hatari zaidi ya Jean Baleke na kiungo atakayekuwa mbadala wa Clatous Chama.

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya timu hiyo, kutolewa na Wydad Casablanca kwa mikwaju wa penalti katika mchezo wa mwisho wa hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba ilitolewa na Wydad Casablanca kwa mikwaju ya penalti katika mchezo huo baada ya kila timu kushinda nyumbani kwake bao 1-0.

nsi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa mara baada ya mchezo huo, haraka kocha huyo alifanya kikao na baadhi ya Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, waliosafiri na kikosi hicho.

Ally alisema kuwa anaamini ubora wa wachezaji lakini, maboresho makubwa yanahitaji katika kuelekea usajili wa msimu ujao, ameomba asajiliwe straika mwenye uwezo zaidi ya Baleke.

Alisema kuwa kocha huyo anapata ugumu wa kupata matokeo kimbinu, kutokana na kuwepo mshambuliaji mmoja pekee tishio kwa wapinzani ambaye ni Baleke pekee.

Aliongeza kuwa pia kocha huyo katika kikao hicho ametoa mapendekezo ya kusajiliwa kiungo mshambuliaji mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza mabao kwa wenzake zaidi ya Chama.

“Baada ya mchezo wa marudiano dhidi ya Wydad Casablanca, kocha Robertionho alifanya kikao na viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi tukiwa hotelini Nigeria.

“Kikubwa ni kutoa tathimini ya timu hiyo, katika ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Afrika na katika kikao hicho ametoa mapendekezo ya usajili wa wachezaji wapya.

“Lengo ni kutengeneza timu itakayokuwa bora na tishio katika Ukanda huu wa Afrika na zaidi kufika hatua ya Nusu Fainali hadi Fainali baada ya misimu mitatu kuishia Robo,” alisema Ally.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz