Pluijm: Kucheza na Yanga ujipange - EDUSPORTSTZ

Latest

Pluijm: Kucheza na Yanga ujipange

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha wa Singida Big Stars, Hans Pluijm amezungumzia namna ubora wa wachezaji wa Yanga unavyowaumiza kichwa wanapokwenda kukutana kwenye nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).


Singida BS imepoteza michezo miwili mfululizo ya Ligi Kuu Bara ikianza na Yanga ikifungwa mabao 2-0 pamoja na ule wa KMC waliofungwa mabao 2-0.


Mei 21, Singida BS wataikaribisha Yangwa kwenye Uwanja Liti, mkoani Singida, hivyo wana mtihani mkubwa wa kuifunga Yanga ambao tayari ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara.


Akizungumza Pluijm alisema kucheza na timu kama Yanga inakubidi utumie mbinu za hali ya juu ili uweze kuwafunga.


Alisema kwa upande wa wachezaji hawatakiwi kurudia makosa ili kushinda mchezo huu, kwani lolote linaweza kutokea kama wakiamua kushinda au kushindwa.


"Michezo iliyopita ikiwemo na KMC tulishindwa kwani kuna baadhi ya wachezaji niliwapumzisha ndio maana niliwachezesha baadhi yao nafasi nyingi na wengine kuwa na kadi za njano,"


"Tunakwenda kucheza kwa nguvu na ubora wote bila kupoteza nafasi kama mchezo uliopita dhidi yao hivyo tutabadilisha mambo."


Chanzo: Mwanaspoti



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz