Ni Yanga vs USM Alger fainali CAF CC - EDUSPORTSTZ

Latest

Ni Yanga vs USM Alger fainali CAF CC

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Wananchi wana dakika 180 za kuwania ubingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya ushindi wa jumla wa mabao 4-1 dhidi ya Marumo Gallants katika mchezo wa nusu fainali


Jana Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Marumo katika mchezo wa nusu fainali mkondo wa pili uliopigwa Afrika Kusini huku pia ikishinda mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa wiki iliyopita


Yanga itachuana na USM Alger (USMA) katika hatua ya fainali baada ya Waarabu hao kutoka Algeria kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya ASEC Mimosas katika mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali uliopigwa huko Algeria


Timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa nusu fainali mkondo wa kwanza huko Ivory Coast


Fainali hii itakuwa kisasi kwa Yanga, Wananchi wakiwa na kumbukumbu ya timu hizo kukutana kwenye michuano hii hatua ya makundi mwaka 2018


USMA waliifunga Yanga 4-0 katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi uliopigwa Algeria na Yanga kushinda 2-1 katika mchezo wa marudiano


Wakati huo Yanga ilikuwa ikinolewa na kocha Mwinyi Zahera aliyetua kuchukua nafasi ya George Lwandamina ambaye alirejea kunako klabu yake ya zamani Zesco United


Mchezo wa fainali mkondo wa kwanza utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa May 28 na marudiano kupigwa Algeria Juni 03Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz