Ni dakika 270 za rekodi kwa Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Ni dakika 270 za rekodi kwa Yanga

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Marumo Gallants katika mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Yanga itasafiri kwenda Afrika Kusini baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa uwanja wa Azam Complex, Jumamosi, May 13


Yanga inaweza kwenda Afrika Kusini ikiwa tayari imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kama itapata ushindi katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji


Hili ni jambo muhimu kwa Wananchi kuhakikisha linakamilika ili kuwekeza nguvu katika mechi mbili zitakazofuata


May 17 Yanga itacheza na mchezo wa marudiano dhidi ya Marumo Gallants katika uwanja wa The Royal Bafokeng huko Afrika Kusini


Baada ya mchezo huo Wananchi watarejea Tanzania kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Singida BS ambao utapigwa May 21 katika uwanja wa LITI, Singida


Yanga ina dakika 270 za kuweka rekodi ya aina yake kwenye soka la Tanzania ambazo ni kutwaa taji la Ligi Kuu kwa mara ya 29, kutinga fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika na pia kutinga fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)


Zaidi Yanga inawania rekodi ya kushinda mataji manne msimu huu Ngao ya Jamii (tayari), Ligi Kuu, CAF CC na ASFCDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz