Nabi awafanyia ushushushu Waarabu - EDUSPORTSTZ

Latest

Nabi awafanyia ushushushu Waarabu

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kama unahisi Yanga itaingia kizembe kwenye mechi mbili za fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, sahau kwani tayari kocha mkuu wa timu hiyo, Nassredine Nabi ‘Profesa’ ametuma makachero kuwasoma wapinzani wao, USM Alger na kuwataka wamletee ripoti kamili haraka iwezekanavyo.


Makachero hao sio wale wa usalama bali ni wataalamu wa soka ambao kazi yao ni kuwasoma wapinzani, kutathimini kikosi chao, ubora wao, wachezaji wa kuchungwa, aina yao ya kucheza wakiwa na mpira na hata wasipokuwa na mpira.


Nabi alifanya hivyo juzi usiku baada ya kumalizika kwa mechi ya USM Alger na Asec Mimosas pale Algeria na kujua atakutana fainali na Alger.


Moja ya watu wa karibu na Nabi tuliyekuwa wote hapa Rustenburg Afrika Kusini alilipenyezea Mwanaspoti kuwa baada ya mechi y Alger na Asee kumalizika, Nabi aliwaita wataalamu wote wa benchi la ufundi usiku na kukaa nao kikao wakijadili njia za kuimaliza Alger ndipo likaja wazo la kutumia makakachero walionao.


Benchi la ufundi la Yanga linaamini ili kupata haraka mikanda kamili ya mechi za Alger na tathimini fupi ya timu hiyo linatakiwa kutafuta wataalamu kutoka Alger wanaoijua vyema timu hiyo ili kupata kiuhalisi mafaili wanauoyahitaji kisha kuyaweka mezani kuyandia mpango mkakati jambo ambalo hadi saaa linaenda vizuri.


Akizungumza nchini Afrika Kusini, Nabi alisema amefurahishwa na kutinga fainali na sasa anajipanga kuhakikisha anachukua ubingwa.


“Wachezaji wangu wamejituma na kufuata maelekezo na mwisho tumetimiza lengo. Tumefirahi kufika hapa na sasa tunaanza safari mpya kuhakikisha tunatwaa ubingwa,” alisema Nabi na kuongeza;


“Mechi za ubingwa hazitakuwa rahisi lakini naamini tunaweza kuzicheza na kuzishinda.


Kwa sasa tunatudi uwanja wa mazoezi na kufanyia tathimini timu tutakayokutana nayo na kuanza kujifua ili kuikabili na kushinda,” alisema kocha huyo aliyeipa Yanga ubingwa wa Ligi katika misimu miwili mfululizo. Mechi ya kwanza ya fainali itapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Mei 28 mwaka huu na marudio Yanga itakuwa ugenini Algeria Juni 3,3023.


Chanzo: Mwanaspoti



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz