Morrison, Gadiel watajwa kujiunga Singida Big Stars - EDUSPORTSTZ

Latest

Morrison, Gadiel watajwa kujiunga Singida Big Stars


 Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Klabu ya Singida Big Stars imeahidi kufanya usajili mkubwa na wenye tija kwa ajili ya kufanya vizuri katika msimu ujao ambao watashiriki mashindano ya kimataifa kwa kuwanasa, Bernard Morrison wa Yanga na Gadiel Michael anayeichezea Simba, imeelezwa.


Hata hivyo tetesi zinasema klabu hiyo iko katika mchakato wa kumwachia kiungo mshambuliaji wake, Bruno Gomes ambaye anawindwa na Simba na Yanga.


Ofisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Masanza, alisema jana wamejipanga kufanya usajili bora kwa sababu tayari wana uhakika wa kuiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la Shirikisho na wanataka kufika mbali na si kusindikiza.


"Tuko katika mkakati mkubwa wa kuboresha kikosi chetu kwa sababu tayari tuna nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa, Kombe la Shirikisho msimu ujao, tutakwenda kufanya usajili wa wachezaji bora wa ndani na nje ya nchi, sisi huwa hatukosei, wote wanajua, huwa tunaleta vifaa haswa," alisema Masanza.


Kuhusu mchezaji Bruno kuondoka katika klabu hiyo msimu huu, alisema haiwezekani wamwachie mchezaji bora kama huyo wakati wanakwenda kucheza mechi za kimataifa.


"Unakwenda kucheza mechi za kimataifa, halafu unamwacha Bruno? Hapana bado ataendelea kuwapo katika timu yetu kwa sababu na sisi tunataka kufanya vizuri siyo kusindikiza," Masanza alisema.


Alikataa kuthibitisha habari za kuwasajili wachezaji wataotajwa msimu ujao watatumikia kikosi hicho.


"Hao ni wachezaji wa timu nyingine, siwezi kuwazungumzia wachezaji wa klabu nyingine na usajili bado haujaanza, kila kitu kikiwa sawa tutawaeleza sisi wenyewe mchezaji yupi tumemsajili," alisema kiongozi huyo.


Singida Big Stars imepata tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao kutokana na kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu, huku timu zilizoingia fainali katika Kombe la FA, Yanga na Azam, nazo tayari zina tiketi ya kucheza michuano ya kimataifa msimu ujao.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz