Matchday : Singida BS vs Yanga, NBC PL Itazame hapa - EDUSPORTSTZ

Latest

Matchday : Singida BS vs Yanga, NBC PL Itazame hapa

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa ambapo mkoani Singida walima alizeti wa Singida BS watakuwa uwanja wao wa nyumbani LITI kuchuana na mabingwa watetezi Yanga


Singida BS wako katika vita ya kuwania nafasi ya tatu hivyo ni wazi watazihitaji alama zote tatu mbele ya Yanga ili kurejea nafasi hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na Azam FC


Hata hivyo wanachuana na Yanga ambayo hesabu imeelekeza kwenye kutetea ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo


Kimahesabu Yanga inahitaji kushinda mechi mbili tu kati ya nne zilizosalia ili kutetea ubingwa


Kama Wananchi watashinda leo basi watakuwa na deni la alama tatu tu ili kutetea ubingwa wao na wanaweza kufanikisha hilo katika mchezo utakaofuata dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa dimba la Azam Complex, jijini Dar es salaam


Baada ya watani zao Simba kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo Fc jana, Yanga inaweza kunufaika na kuteleza huko kwa watani zao kama itashinda leo


Mchezo utapigwa saa 10 jioni katika uwanja wa LITI Mechi itakuwa LIVE kwenye app yetu bofya hapa kuidownload bure sasaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz