Majeruhi 18 wameruhusiwa hospitali ya Temeke kufuatia vurugu kwa Mkapa - EDUSPORTSTZ

Latest

Majeruhi 18 wameruhusiwa hospitali ya Temeke kufuatia vurugu kwa Mkapa

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana amewajulia hali majeruhi 10 wanaoendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya Temeke waliojeruhiwa kutokana na tukio la kukanyagana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wakijiandaa kuingia kutazama mechi kati ya Yanga na USM Alger ya nchini Algeria katika mchezo wa Kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, uliocheza Mei 28, 2023.


Chana alipokea taarifa kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Joseph Gasper Kimaro kwamba, walipokea majeruhi 30 ambapo wanaume walikua 18, Wanawake 10 na mtoto Mmoja ambapo mgonjwa mmoja alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu.


Ameeleza kuwa mpaka sasa wamebakiwa na wagonjwa 10 na wote wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea  kuimarika.


Chana katika ziara hiyo aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, Katibu Mkuu, Saidi Yakubu, Mkuu wa Wilaya, Mwanahamisi Munkunda.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz