Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ Adel Amrouche amewasili katika kambi ya Yanga iliyopo Rustenburg, Afrika Kusini saa chache kabla ya kuanza kwa mechi ya nusu fainali, Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na wenyeji Marumo Gallants.
Amrouche alivyowasili alipokelewa na baadhi ya viongozi wa Yanga na kuendelea na mazungumzo huku akitarajiwa kuungana na msafara utakaokwenda uwanjani hapo baadae.
Kocha huyo licha ya sababu nyingi za kuwepo kambini hapo lakini kubwa zaidi amekuja kuwatazama wachezaji Watanzania walio katika klabu ya Yanga.
Amrouche atakuwa uwanjani wakati wa mechi na mbali ya kutazama mchezo, atakuwa akifanya tathimini ya wachezaji watanzania kwaajili ya Taifa Stars.
Yanga hapa Afrika Kusini ipo na jumla ya wachezaji 23 lakini Watanzania ni makipa, Metacha Mnata na Eric Johora.
Mabeki, Shomari Kibwana, Dickson Job, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ na Bakari Mwamnyeto, Viungo Zawad Mauya, Salum Abubakari ‘SureBoy, Mudathir Yahya, Farid Mussa, Denis Nkane, na mshambuliaji Clement Mzize.
Ikumbukwe Amrouche anakaribia kuita kikosi cha Stars kitakachoingia kambini kujiandaa na mechi za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon).
No comments:
Post a Comment