Huyu hapa mwamuzi wa mechi ya Yanga vs Usm Alger - EDUSPORTSTZ

Latest

Huyu hapa mwamuzi wa mechi ya Yanga vs Usm Alger

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Refa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jean-Jacques Ngmbo Ndala ndiye atakayechezesha Fainali ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumapili wiki hii Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.


Ngmbo Ndala atasaidiwa na Mkongo mwenzake Olovier Kabene Safar na Zakhele Thusi Granville Siwela wa Afrika Kusini watakaokuwa wanakimbia na vibendera pembezoni mwa Uwanja kulia na kushoto.


Mchezo wa marudiano utafuatia Juni 3 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) litatoa orodha nyingine ya waamuzi.


Kufika hatua hii, Yanga imeitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-1, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini, wakati USM Alger imeitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast baada ya sare ya 0-0 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz