Hii hapa taarifa mpya kutoka yanga ni kuhusu ujenzi wa uwanja wa Yanga ulipofikia mpaka sasa - EDUSPORTSTZ

Latest

Hii hapa taarifa mpya kutoka yanga ni kuhusu ujenzi wa uwanja wa Yanga ulipofikia mpaka sasa

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema klabu imeanza mchakato wa ujenzi wa uwanja eneo la Jangwani yalipo Makao Makuu ya klabu ya Yanga


Akizungumza katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, Injinia Hersi alisema taratibu za awali zimeshaanza kufanyika hapo Jangwani


"Kuhusu ujenzi wa Uwanja tuna kiwanja Kigamboni lakini pia tuna eneo ambalo lina jengo la Klabu pale Jangwani, sisi binafsi tumependelea kujenga uwanja wetu pale Jangwani na tayari taratibu zimeshaanza katika kulitekeleza hilo," alisema Hersi


Ujenzi wa uwanja ilikuwa moja ya ajenda za Injinia Hersi wakati akigombea Urais wa klabu ya Yanga


Moja ya sababu ambayo Hersi aliitaja kujenga uwanja pale Jangwani badala ya Kigamboni ambako Yanga ina eneo kubwa zaidi, ni urahisi wa kufikika kwa mashabiki


Hersi alisema wataalam waliwathibitishia kuwa katika eneo lao la uwanja wa zamani wa Kaunda, wanaweza kujenga uwanja wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 20,000Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz