Fei Toto Afunguka Tena "Nimemisi Kufunga na Mashooti Yangu ya Mbali, Nisaidieni Jamani" - EDUSPORTSTZ

Latest

Fei Toto Afunguka Tena "Nimemisi Kufunga na Mashooti Yangu ya Mbali, Nisaidieni Jamani"

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Baada ya juhudi za Mchezaji Feisal Salum “Fei Toto” kugonga mwamba mara mbili TFF kwa kushindwa kukubaliwa ombi lake la kuvunja mkataba na Yanga na Mchezaji huyu juzi kutangaza kuomba msaada wa pesa kwa Watanzania ili aweze kwenda kwenye Mahakama ya usuluhishi wa kimichezo (CAS), leo tena amekazia ombi lake na kuomba Watu wamchangie ili arudi uwanjani.

Feisal ameandika yafuatayo katika taarifa yake “Ndugu zangu Watanzania, natamani kurdi uwanjani na kuendelea kuwafurahisha wapenda soka, nimebakisha hatua chache, nisaidieni niweze kukamilisha nia yangu ya kwenda CAS na kupata haki ya kurudi tena uwanjani”

“Nimekumbuka nyakati bora, nimekumbuka kupiga mashuti yangu ya mbali, nimekumbuka kufurahia na Mashabiki wa soka, Fei Toto ni mmoja tu, msaidie arudi uwanjani kwa haki inayotaka kudhulumiwa”

“Unaweza kulipia kwa lipa namba (5406394 FEISAL SALUM) hapo pichani au kwa namba hii ya simu kwa kwa Tigo Pesa 067 912 8899 FEISAL SALUM ABDALLAH, aidha natoa pole kwa kifo cha Shabiki wa Soka na majeruhi katika kadhia ya Jana, ALLAH ATAWAPONYA INSHALLAHl”


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz