Yanga yapania kufika nusu fainali kombe la shirikisho CAF - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga yapania kufika nusu fainali kombe la shirikisho CAF

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kuendelea kununua tiketi kwa wingi kuelekea mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United


Kesho Jumapili Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili Rivers United katika mchezo ambao Yanga inahitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare kutinga nusu fainali ya kwanza


"Itakuwa heshima na kumbukumbu kwa shabiki kuwa uwanjani pale Yanga inapofuzu kwenda nusu fainali. Miaka mingi ijayo mtajivunia kwa vizazi na wajukuu zenu kuwa mlikuwepo uwanjani wakati Yanga ikiandika historia kubwa kwa nchi"


"Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu lakini naamini ushindi wa mabao 2-0 tuliopata ugenini umetuweka katika nafasi nzuri. Wachezaji wetu wako tayari na wameahidi watapambana kuhakikisha tunashinda"


"Wito wao kwenu mashabiki ni kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwaongezea hamasa," alisema Kamwe


Baada ya Simba kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa jana, Yanga ndio klabu pekee inayoendelea kupeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya CAFDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz