USAJILI: Huyu hapa beki kitasa anayetajwa kuwindwa na Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

USAJILI: Huyu hapa beki kitasa anayetajwa kuwindwa na Simba

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kutokana na makosa ambayo yanafanywa na safu ya ulinzi ya Simba kwenye mechi za kimataifa, Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amewataka wachezaji wake kuongeza umakini huku beki wa Cape Town City ya Afrika Kusini, Nathan Idumba Fasika akitajwa kuwa njiani kutua kikosini hapo.

Idumba alijunga na Cape Town City Julai 16, 2021 akitokea FC Saint Eloi ya kwao DR Congo, ambapo mkataba wake na Cape Town unatarajiwa kufikia kikomo Juni 30, 2026.

Hivi karibuni, Kocha wa Simba aliweka wazi kuwa safu yake ya ulinzi imekuwa na makosa mengi kuanzia michuano ya ndani hadi ya kimataifa.

Sasa safu hiyo inayoongozwa na Joash Onyango pamoja na Henock Inonga imetengeneza penalti tatu zote zikitengenezwa na Onyango kwenye harakati za kuokoa hatari katika michuano ya kimataifa msimu huu.

Kutokana na hilo, chanzo kutoka Simba kimeliambia Championi Jumatano kuwa, kutokana na Kocha wao raia Brazil, Robertinho kuendelea kusisitiza kuongeza beki wa kati, wanatarajia sasa kumalizana na Idumba ili kupunguza presha kwenye eneo hilo.

“Tunalazimika tena kutafuta beki mwingine atakayekuja kuongeza nguvu kikosini, jambo ambalo linatufanya kurejea mezani kuzungumza na uongozi wa Cape Town ili tumpate Idumba.

“Nadhani unakumbuka mwanzo tulizungumza naye pamoja na timu yake ila dau likawa kubwa tukaamua kumsajili Mohamed Ouattara ambaye kocha bado haridhishwi naye jambo ambalo linatufanya tuingie sokoni tena kupata hitaji la kocha,” kilisema chanzo hicho.

Championi lilizungumza na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ambapo alisema:

“Tumepanga kufanya usajili mkubwa kwa ajili ya msimu ujao, zaidi tutaangalia wale wachezaji ambao wanacheza mara kwa mara na sio wale wa historia, hivyo dirisha likifunguliwa hayo ndiyo malengo ila kwa sasa bado hatujaingia rasmi kwenye usajili.”

Chanzo: Gazeti la champion 


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz