"Tutawapa furaha mashabiki wetu" Djuma - EDUSPORTSTZ

Latest

"Tutawapa furaha mashabiki wetu" Djuma

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kikosi cha Yanga kilitua Mji wa UYO huko Nigeria jana na kuanza maandalizi yake kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United


Mchezo huo utapigwa kesho Jumapili April 23 katika uwanja wa Godwill Akpabio, moja ya viwanja vyenye 'pitch' nzuri ndani ya Nigeria


Beki wa kulia wa Yanga, Djuma Shaban 'Soja ya Bemba', amesema kama kuna maumivu makubwa katika mioyo yao ni juu ya matokeo ya kupoteza dhidi ya watani wao Simba lakini wamepania kubadilisha upepo kupitia mchezo dhidi ya Rivers United


Djuma amesema wanajua ubora wa wenyeji wao wakikutana nao mara ya pili ingawa wanafahamu kwamba wana kikosi kipya lakini kwasasa tayari wanawajua juu ya udhaifu wao na ubora wao


"Tuliwaumiza mashabiki wetu na sisi imetuuma sana kufungwa na Simba lakini hayo yamepita sasa umebaki ujumbe wa kutukumbusha kwamba tunatakiwa kubadilisha yale matokeo ili tuwarudishie furaha watu wetu,"alisema Djuma


"Tumeangalia mechi zao tunajua sasa wapi tupatumie kutengeneza ushindi lakini pia tutaongeza umakini kuhakikisha tunawazuia washambuliaji wao ambao wana ubora ili wasiharibu hesabu zetu"


Baada ya mchezo huo wa mkondo wa kwanza, Yanga itarejea jijini Dar es salaam kukamilisha mchezo wa pili utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, April 30Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz