Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mabosi wa timu hiyo wameingia kwenye hofu kubwa ya kukosa kipa huyo namba mbili kufuatia Kakolanya kutajwa kujiunga na Singida Big Stars kwa mkataba wa miaka miwili kufuatia mkataba wake na Simba kufikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu.
Hofu ya mabosi hao imekuwa baada ya kipa huyo kutokuwa kwenye msafara wa Simba uliokuwepo kwenye mchezo juzi Jumatatu dhidi ya Ihefu ambao timu hiyo ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo zinaeleza kuwa mabosi wa timu hiyo ambao kwa sasa ameanza kupambana kuhakikisha anabakia kwenye timu huku yeye akitoa masharti yake.
“Ni kweli Kakolanya amezua hofu kwa mabosi wa juu kwa sababu wameshajua kama amesaini mkataba na Singida na tayari ameshawekewa pesa ambayo wamekubaliana na kinachosubiliwa ni ligi kumalizika ili aweze kujiunga nao.
“Lakini wamekuwa na mazungumzo na kipa mwingine wa kigeni kutoka nje kama itashindikana kumrudisha Kakolanya kwa kurudisha pesa alizochukua basi watamchukua huyo kipa ingawa Kakolanya amewapa masharti yake ikiwa wanataka abakie kwenye timu,” alisema mtoa taarifa.
Baada ya kumtafuta Meneja wa Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa kwa sasa suala hilo bado halijafika kwenye meza yake hivyo hawezi kuzungumzia chochote.
“Binafsi bado halijafika kwenye mezani yangu kwa sababu pengine linashughulikiwa na uongozi wa juu ila kwa sasa sijui chochote juu ya jambo hilo,” alisema Ally.
Post a Comment