Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Chelsea imefanya mawasiliano na mkufunzi wa zamani wa Bayern Munich Julian Nagelsmann, 35, na meneja wa zamani wa Uhispania Luis Enrique, 52, juu ya kuwa meneja mpya wa klabu hiyo. (Telegraph - Subscription Required)
Bosi wa Brighton Muitaliano Roberto de Zerbi, 43, hatachukuliwa kuwa meneja anayetarajiwa wa Chelsea baada ya kutimuliwa kwa Graham Potter. (Subscription Required)
Mwingereza Potter, mwenye umri wa miaka 47, anawania kuwa kocha anayefuata wa West Ham huku klabu hiyo ikitarajiwa kufikiria mustakabali wa meneja wa sasa, Scot David Moyes, 59, msimu wa joto. (Telegraph - Subscription Required)
Wote De Zerbi na Nagelsmann wameonyesha kutovutiwa na kazi iliyo wazi ya meneja wa Tottenham. ( 90min)
Meneja wa zamani wa Crystal Palace, Mfaransa Patrick Vieira, 46, anaweza kuwa meneja wa Nottingham Forest ikiwa klabu hiyo itaamua kumfukuza Mwingereza Steve Cooper, 43. (Mail)
Mshambulizi wa Argentina Lionel Messi, 35, huenda asifikie makubaliano na Paris St-Germain kuongeza muda wake wa kusalia katika klabu hiyo. (ESPN)
Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia imetoa ofa rasmi kwa Messi yenye thamani ya zaidi ya euro 400m (£350m) kwa mwaka. (Fabrizio Romano)
Manchester United, Liverpool na Tottenham wameonyesha nia ya kuamsha kifungu cha pauni milioni 40 cha kumtoa beki wa Napoli wa Korea Kusini Kim Min-jae, 26. (Mail).
Liverpool wameelekeza mawazo yao kwa kiungo wa kati wa Brighton na Ecuador Moises Caicedo, 21, baada ya Wolves kuondoa kipengele kutoka kwa kiungo wa kati wa Ureno Matheus Nunes ambacho kingewaruhusu The Reds kufanya ununuzi wa kumnunua mchezaji huyo wa miaka 24 kwa pauni milioni 44 msimu huu. (Mirror)
Wolves wanajiandaa kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Dani Ceballos, huku mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 26 ukimalizika msimu huu. (90min)
Ajax wana nia ya kumrejesha kiungo wa kati wa Manchester United na Uholanzi Donny van de Beek, 25, katika klabu hiyo msimu huu. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 23, atakuwa tayari kujiunga na Arsenal msimu huu wa joto, baada ya kuwakataa The Gunners kwa Juventus Januari mwaka jana. (Four Four Two)
Liverpool itamruhusu kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita, 28, kuondoka katika klabu hiyo kwa uhamisho wa bila malipo msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)
Sampdoria haitafanya mkataba wao wa mkopo kwa kiungo wa kati wa Tottenham na Uingereza Harry Winks, 27, kuwa wa kudumu kutokana na matatizo ya kifedha katika klabu hiyo. (Sun)
Leicester, Aston Villa, Brentford, Brighton na Crystal Palace wanavutiwa na mshambuliaji wa Feyenoord Santiago Gimenez, huku klabu za Italia, Ufaransa na Ujerumani pia zikimfuatilia mchezaji huyo wa Mexico mwenye umri wa miaka 21. (90min)
BBC
Post a Comment