Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Liverpool wamemfanya Mason Mount wa Chelsea , 24, kuwa kiungo wa kati anayelengwa msimu huu baada ya kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mchezaji mwenzake wa Uingereza Jude Bellingham, 19, kutoka Borussia Dortmund.(Football London)
Bayern Munich wanafikiria kuwasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, ambaye yuko tayari kuhamia klabu hiyo ya Bundesliga. (Sky Germany - kwa Kijerumani) Mkufunzi wa zamani wa River Plate Marcelo Gallardo anagombea nafasi ya meneja wa kudumu katika klabu ya Chelsea . (UOL - kwa Kireno)
Mchakato wa zabuni ya kuinunua Manchester United unaingia raundi ya tatu huku wamiliki wa sasa - Glazers wakishikilia kutaka ofa ya karibu £6bn(Mail)
Newcastle ni miongoni mwa klabu kadhaa za ligi ya premier zilizo tayari kumnunua winga wa Leicester mwenye umri wa miaka 25 Muingereza Harvey Barnes ikiwa Foxes watashuka daraja kutoka ligi kuu.(Football Insider)
Kiungo wa kati wa Manchester City na Ireland Kaskazini Shea Charles, 19, analengwa na Leeds, Brentford na Borussia Dortmund . (Guardian)
Real Madrid wanafikiria kumsajili fowadi wa Brazil Roberto Firmino, 31, kwa uhamisho wa bila malipo mkataba wake wa Liverpool utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (El Nacional - kwa Kihispania)
West Ham inalenga kuwasajili Conor Gallagher, 23, wa Chelsea na Kalvin Phillips wa Manchester City , 27, kama wanaoweza kuziba nafasi ya kiungo mwenza wa Uingereza Declan Rice, 24. (Standard)
Kiungo wa kati wa Ireland Kaskazini Isaac Price, 19, anakaribia kusaini mkataba wa awali katika klabu ya Standard Liege baada ya kukataa kandarasi mpya na Everton . (Liverpool Echo)
Wolves inaandaa ofa mpya ya kandarasi kwa kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, 26, ambaye hapo awali alikuwa akihusishwa na Arsenal na Manchester United. (Sun)
Mawakala wa mlinda lango wa Valencia na Georgia Giorgi Mamadashvili, 22, walifanya mazungumzo na Chelsea, Tottenham, Manchester United na Leicester wiki iliyopita(90Min)
Arsenal wanataka kumsajili winga wa Flamengo mwenye umri wa miaka 17 raia wa Brazil Matheus Goncalves (Sun)
Nottingham Forest wamefanya mazungumzo na mkurugenzi wa michezo wa Rangers Ross Wilson ili kutafuta mbadala wa Filippo Giraldi..(Athletic - usajili unahitajika)
BBC
Post a Comment