Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumamosi - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumamosi

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Chelsea wameingia katika mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, msimu huu. (Evening Standard)


Chelsea pia wanajipanga kuwasilisha ombi la kumnunua beki wa kushoto wa Barcelona na Hispania Alejandro Balde, 19, kuchukua nafasi ya beki wao wa England Ben Chilwell, 26. (Sport).


Bayern Munich wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Kai Havertz, 23, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani akionyesha nia ya kuungana tena na meneja wake wa zamani Thomas Tuchel. (90Min)


Paris St-Germain wamemwambia Lionel Messi kwamba watalipa chochote kinachohitajika ili kumbakisha mshambuliaji huyo wa Argentina, 35, huku kukiwa na ripoti kwamba Barcelona wamewasiliana na Messi kuhusu uwezekano wa kurejea. (Mundo Deportivo)


Arsenal wanamtaka kiungo wa kati wa Real Madrid Aurelien Tchouameni kuboresha kikosi chao msimu wa joto, huku Liverpool pia ikidaiwa kumtaka Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 23. (El Nacional)


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alisema klabu hiyo imekuwa na shughuli nyingi wakati wa mapumziko ya kimataifa ikipanga malengo ya msimu wa joto na iko tayari kutumia pesa nyingi katika soko la usajili. (Mirror)


Mshambulizi wa Chelsea Pierre-Emerick Aubameyang, 33, anataka kurejea Barcelona lakini The Blues hawataki kumuuza mshambuliaji huyo wa Gabon. (Sport)


Roma wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa Manchester United David de Gea, huku Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 32 mkataba wake ukikamilika msimu wa joto. (Fichajes)


Wachezaji wawili wa Crystal Palace na Ghana Jeffrey Schlupp, 30, na Jordan Ayew, 31, wametia saini kandarasi mpya huko Eagles. (Athletic)


BBCDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz