Simba wataja Sababu ya Moses Phiri kutopangwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba wataja Sababu ya Moses Phiri kutopangwa

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Benchi la ufundi la Simba limeweka wazi kuwa sababu ya mtambo wao wa mabao, Moses Phiri kujenga ushikaji na benchi ni kutokuwa fiti asilimia 100 baada ya kupata maumivu.


Phiri katupia mabao 10 kibindoni kwenye ligi akiwa ni namba moja kwa utupiaji upande wa Simba na ametengeneza pasi tatu za mabao. 


Baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba, Phiri alikuwa nje kwa muda akipambania afya yake na kwa sasa tayari amesharejea lakini bado hajawa na uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza.


Juma Mgunda, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa Phiri ni mchezaji mzuri lakini bado hajarejea kwenye uimara wake asilimia kubwa. 


“Phiri ni mchezaji mzuri tangu alipopata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar bado hajarejea kwenye ule ubora wake hivyo taratibu anazidi kuimarika tuna amini atarejea kwenye ubora wake.”Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz