Sikia Tambo za kocha wa Yanga Nasreddine Nabi - EDUSPORTSTZ

Latest

Sikia Tambo za kocha wa Yanga Nasreddine Nabi

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi wamejifungia Avic Town kukamilisha maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba abao utapigwa Jumapili, April 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa


Kila Mwananchi anafahamu umuhimu wa mchezo huu ambapo matokeo ya ushindi yatakuwa yameihakikishia Yanga ubingwa kwa zaidi ya asilimia 80


Nabi anajivunia ubora wa kikosi chake akiamini maandalizi yao yatatosha kuwafanya wawe na ubora mkubwa kwenye mchezo huo


"Tunawaheshimu Simba ni timu yenye mabadiliko lakini hatuwezi kuwa na presha hata kidogo, tunakwenda kuandaa timu ambayo itakuja uwanjani kucheza kwa ubora mkubwa kwenye mechi hii kubwa, tunawajua vizuri sana," alisema Nabi


Profesa Nabi tangu ajiunge na Yanga April 2021, ndani ya mechi 8 za mashindano yote dhidi ya Simba ameshinda 4 akipoteza 1 na kutoa sare 3


"Kitu bora kwetu wachezaji ambao walikuwa majeruhi wamerejea, hii itatupa nafasi pana ya kuchagua nani anaweza kuwa ndani ya kikosi kuelekea mchezo huo"


"Malengo yetu ni kuendelea kushinda, tunahitaji ushindi ili kuendelea kuweka hai malengo ya kuchukua ubingwa wakati kama huu ni vyema kuongeza pointi na sio kupunguza"


"Narudia tunaiheshimu Simba na hautakuwa mchezo rahisi lakini niseme Yanga itaingia uwanjani kucheza kwa ubora mkubwa kwa ujazo wa mchezo mkubwa kama huo ili tupate ushindi, jambo la msingi kwetu ni kushinda," aliongeza Nabi
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz