Real Madrid, Ac Millan zatinga nusu Fainali UEFA - EDUSPORTSTZ

Latest

Real Madrid, Ac Millan zatinga nusu Fainali UEFA

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Chelsea imeondoshwa kwenye Ligi ya Mabingwa kwa kupoteza kwa jumla ya mabao 4-0 kutoka kwa mabingwa watetezi Real Madrid


Mabao mawili ya Rodrygo yalitosha kuwaadhibu The Blues kwa kichapo cha 2-0 Stamford Bridge huku yakiwashuhudia Real Madrid wakitinga nusu fainali katika michuano ambayo imekuwa kawaida yao kushinda wanapofika hatua hiyo


Kikosi cha Frank Lampard kilihitaji kupindua kipigo cha mabao mawili kutoka kwa mechi ya kwanza ili kuwa na matumaini lakini haikuwezekana 


Ilikuwa mechi ya nne mfululizo Lampard anapoteza tangu akabidhiwe mikoba ya kuwa kocha wa muda


AC Milan nao wakawaduwaza mabingwa watarajiwa wa Serie A Napoli kwa kuwalazimisha sare ya bao 1-1 katika uwanja wao wa nyumbani


Milan wametinga nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 kufuatia ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa San Siro


Mechi nyingine mbili za robo fainali zitapigwa leo, Bayern Munich wakiwa nyumbani watakuwa na kazi ya kupindua matokeo ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Manchester City wakati Inter Milan watahitaji kulinda ushindi wa mabao 2-0 waliopata ugenini dhidi ya Benfica



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz