Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mabingwa watarajiwa wa Serie A Napoli jana walipata kichapo cha tatu msimu huu wakibomolewa mabao 4-0 na mabingwa watetezi AC Milan
Vijana wa Luciano Spalletti wanaendelea kuongoza ligi mbele ya Lazio walio nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi 16, huku Milan wakipanda hadi nafasi ya tatu
Rafael Leao alifunga bao la kwanza na Brahim Diaz akaifungia Milan bao la pili. Leao akaweka la tatu kabla ya lexis Saelemaekers akafunga bao la nne
Timu hizo zitakutana tena katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa mwezi huu, tarehe 12 na 18 Aprili
Napoli, ambao wamekuwa bora msimu huu, sasa wamepoteza michezo miwili kati ya minne iliyopita ya Serie A, baada ya kuchapwa katika mechi moja kati ya 24 za kwanza
Lakini bado wanahitaji kushinda mechi tano kati ya 10 zilizosalia za ligi ili kujihakikishia ubingwa wa Serie A tangu 1990
Hiki kilikuwa kipigo chao kikubwa zaidi tangu kufungwa 5-1 na Atalanta mnamo 2007-08
No comments:
Post a Comment