Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Benchi la Ufundi la Namungo FC limesisitiza kuwa tayari kukabili Simba SC katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Mei 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Majaliwa ulioko Ruangwa mkoani, Lindi. Kocha Mkuu wa Namungo, Denis Kitambi, amesema kikosi chake kinaendelea na programu mbalimbali za mazoezi kwa lengo la kujiimarisha ili kusaka ushindi katika mchezo huyo.
Kitambi amesema wanafahamu ubora wa Simba SC na kwa sababu hiyo watacheza kwa tahadhari kubwa na kamwe hawaihofii timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, Dar es Salaam.
“Tunajiimarisha, tunajipanga kumkabili mpinzani wetu ambaye tunajua ametoka kushiriki mashindano ya kimataifa, hatumhofii. Ninaamini kila kitu kitakwenda sawa,” amesema Kitambi.
Ameongeza anaendelea kuyafanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika michezo iliyopita kwa lengo la kumaliza msimu kwa kuzibakisha alama tatu muhimu nyumbani.
“Malengo yangu ni kuhakikisha timu inafamya vyema michezo yote iliyobakia, ninaomba mashabiki wetu waendelee kutupa ushirikiano,” Kitambi amesema.
Ameongeza anaendelea kuwajenga kisaikolojia wachezaji ili wasicheze chini ya kiwango huku akiendelea kushukuru wanaendelea vyema kiafya.
No comments:
Post a Comment