Mchezo wa Yanga unaofuata ni dhidi ya Timu hii - EDUSPORTSTZ

Latest

Mchezo wa Yanga unaofuata ni dhidi ya Timu hii

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mchezo wa derby umeshapita, focus ya Yanga sasa inahamia kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United


Mtanange huu utapigwa Jumapili, April 23 huko Nigeria katika uwanja wa Godswill Akpabio uliopo mji wa Uyo


Rivers United walitumia uwanja huo kwenye hatua ya makundi na baadae wakaomba kuruhusiwa kurejea kwenye uwanja wao wa Adokiye Amiesimaka huko Port Harcort ila Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limegomea mabadiliko hayo baada ya kufanyia ukaguzi uwanja huo na kubaini bado haukidhi vigezo


Yanga itakwenda Nigeria ikiwa na lengo moja, kusaka ushindi ugenini na hata ikishindikana kupata matokeo ya sare


Mchezo wa marudiano utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, April 30 2023


Malengo ya Yanga ni kufuzu nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga inaweza kufunga msimu huu ikiwa na mataji manne 


Iko kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC kwa tofauti ya alama tano dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili zikiwa zimesalia mechi nne tu, pia iko hatua ya nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam, na inasaka nafasi ya kutinga nusu fainali ya kombe la CAF la Shirikisho


Mwanzoni mwa msimu ilitwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz