Matokeo Yanga princess vs Amani queens leo Jumamosi

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Yanga Princess wameibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Amani Queens kwenye mchezo wa Ligi Kuu Ya Wanawake (SWPL) uliomalizika kwenye dimba la Uhuru jioni ya leo.


Mshambuliaji wa kimataifa raia wa Msumbiji, Cuta Ninika “Neymar” alifungua akaunti yake ya magoli akiwa na jezi ya Yanga Princess kwa kufunga magoli mawili na kutoa “assist” moja, akiwa kwenye ubora wa hali ya juu.


Baada ya mchezo huo sasa Princess wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama 20, huku wakihitimisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL), ambapo ligi hio itaenda mapumziko mafupi na kuruhusu wachezaji wengine watakaoenda kwenye kambi za timu zao za taifa.


Ligi hiyo itarejea tarehe 9 Machi ambapo Yanga Princess watakuwa na kibarua kingine dhidi ya Fountain Gates Princess kwenye dimba la Jamuhuri, mkoani Dodoma.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post