Matokeo Simba vs Yanga Leo Jumapili April 16,2023 - EDUSPORTSTZ

Latest

Matokeo Simba vs Yanga Leo Jumapili April 16,2023

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Simba imeondoka na alama zote tatu katika uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga


Kiwango kibovu kwa Yanga dakika 45 za kipindi cha kwanza ziliwagharimu Wananchi wakiruhusu bao mapema tu dakika ya pili Hennock Inonga akitumia vyema makosa ya safu ya ulinzi katika kucheza mpira wa kona


Bao la pili kwa Simba lilifungwa na Kibu Denis kwenye dakika ya 32 baada ya Yanga kupoteza mpira kwenye na kufanyiwa shambulizi la kushitukiza


Kipindi cha pili Yanga ilirejea mchezoni lakini haikuwa rahisi kuipenya ngome ya Simba waliorudi nyuma kujilinda zaidi


Ni mchezo wa pili Yanga inapoteza msimu huu ikiendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi na alama 68 wakati Simba sasa ikisogea ikifikisha alama 63Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz