Match day LIVE: Simba vs Ihefu Fc - EDUSPORTSTZ

Latest

Match day LIVE: Simba vs Ihefu Fc

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Kikosi cha Simba kinashuka kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi leo majira ya saa 1 usiku kucheza na Ihefu Fc katika mchezo wa robo fainali Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)

Simba ilitinga robo fainali kwa kuiondosha African Sports kwa mabao 4-0 huku Ihefu ikiitoa Pan Africans kwa kuichapa 2-0 katika 16 bora ambapo timu zote zikishiriki Ligi ya Championship

Baada ya mechi ya leo, timu hizo zitarudiana tena Aprili 10 kwenye Uwanja wa Highland Estate Mbeya katika mchezo wa ligi kuu huku Ihefu ikikumbuka kupoteza bao 1-0 mara ya mwisho ilipokutana na Simba Novemba 12, mwaka jana.

Simba inatazama kwa jicho la kipekee kwenye michuano hii ikiwania rekodi ya aina yake. Simba ndio mbabe wa ASFC wakitwaa mara tatu tangu michuano hiyo ilipoanzishwa msimu wa 2015-16

Simba ilitwaa taji hilo mwaka 2016-2017, 2019-2020, 2020-2021 huku mara ya mwisho ikishinda na Yanga kwa kuifunga bao 1-0 Julai 25, 2021 Uwanja wa Lake Tanganyika

Kikosi cha kocha Robertinho Oliveira kinawania taji la nne la michuano hiyo msimu huu


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz