"Mashabiki wasubiri Timu Bora " Robertinho - EDUSPORTSTZ

Latest

"Mashabiki wasubiri Timu Bora " Robertinho

 

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Droo ya Robo Fainali ya mashindano ya CAF 2022/23, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika inatarajiwa kufanyika leo Jumatano, Aprili 5, 2023 mjini Cairo, Misri kuanzia saa 03:30 usiku


Droo hiyo itaonyeshwa moja kwa moja kwenye majukwaa ya kidijitali ya CAF na TV washirika. Wakati wadau wa soka nchini wakisubiri kwa hamu droo hiyo ili kujua wapinzani wa Simba na Yanga, Mkufunzi wa Simba Robertinho Oliveira ameanza maandalizi ya kikosi chake malengo ya Simba yakiwa kutinga nusu fainali


Lakini kabla ya mechi hizo za robo fainali CAF zitakazopigwa April 22-28, Simba inakabiliwa na mechi tatu muhimu ambapo moja ya robo fainali kombe la FA dhidi ya Ihefu Fc itakayopigwa Ijumaa April 07, mechi ya ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc itakayopigwa April 10 na mechi ya ligi kuu dhidi ya Yanga itakayopigwa Apripl 16


Robertinho amesema kwa sasa wanajiandaa kwa mechi zinazofuata mbele lakini hawana hofu yoyote kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kwani watakuwa tayari kupambana na timu yoyote watakayopangiwa


"Hatuwezi kuchagua mpinzani wa kukutana naye, yeyote ambaye tutapangwa naye tutakabiliana naye, tunaweza kufanya maajabu na kushangaza Afrika, tutafanya maandalizi hatua kwa hatua, yapo ambayo tuliyaona kwenye makundi tutadili nayo ili kuweka sawa mambo kabla ya hatua ya robo fainali"


"Siku zote nimekuwa na mtazamo chanya hivyo matarajio yangu ni makubwa, yaliyopita yamepita na kazi kubwa ni kuona vile ambavyo tunaweza kuwa bora maradufu hatua inayofuata, tupo pazuri nafikiri mashabiki wasubiri timu bora zaidi robo fainali"


"Tumeshafanya kazi ya kurekebisha makosa na muda tulionao tutamalizia, naamini kwenye ubora wa timu na hilo litatimia," alisema Robertinho


Simba itachuana na Mamelodi Sundowns, Esperance au Wydad Athletic katika hatua ya robo fainali ambapo mpinzani wake atafahamika baada ya droo itakayofanyika leoDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz