Man City waishusha Arsenal kileleni EPL - EDUSPORTSTZ

Latest

Man City waishusha Arsenal kileleni EPL

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mabingwa watetezi, Manchester City wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Fulham leo Uwanja wa Craven Cottage Jijini London.


Mabao ya Manchester City yamefungwa na washambuliaji Mnorway, Erling Haaland kwa penalti dakika ya tatu na Muargentina Julian Álvarez dakika ya 36, wakati la Fulham limefungwa na Carlos Vinícius dakika ya 15.


Kwa ushindi huo, Manchester City imefikisha pointi 76 katika mchezo wa 32 na kurejea juu ya msimamo wakiizidi pointi moja Arsenal ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, huku Fulham ikibaki na pointi zake 45 za mechi 33 nafasi ya 10.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz