Lukaku atupia Inter ikiadhibu BENFICA 2-0

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Inter Milan walitumia dakika 45 za kipindi cha pili kupata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya benfica na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya


Nico Barella na Romelu Lukaku walifunga mabao hayo yanayowaweka mbele Inter kuelekea mechi ya mkondo wa pili utakaopigwa Italia wiki ijayo


Barella alifunga kwa kichwa katika dakika ya 51, akimalizia krosi nzuri kutoka kwa beki wa kati Alessandro Bastoni, ambaye alikuwa akishambulia upande wa kushoto


Lukaku aliyetokea benchi, alifunga penalti dakika ya 82 baada ya VAR kuelekeza mpira uliogonga mkono wa nahodha wa Benfica Joao Mario 


Mabao hayo mawili yanaipa Inter faida kubwa katika mchezo wa marudiano utakaopigwa San Siro Jumatano ijayo, ambapo watakuwa na nafasi kubwa ya kutinga nusu-fainali ya Italia dhidi ya majirani zao AC Milan au Napoli

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post