Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka Wananchi wafurike kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa jioni ya leo katika mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United
Mchezo huo ambao dakika 90 zinaweza kuihakikishia Yanga kutinga nusu fainali, utapigwa saa 1 usiku
"Mashabiki waje kwa wingi na leo tunavaa jezi za njano na kijani, kila mwananchi ahakikishe amezingatia mavazi hayo"
"Wakati timu zinaingia uwanjani, uwanja mzima utasimama kuimba wimbo wa kivumbi na jasho. Pale mechi inapoanza tu, Wananchi wote tuwashe vitochi"
"Lakini baada ya mechi kuna jambo kubwa tumeandaa, tukifuzu. Usiondoke uwanjani kuna surprise," alisema Kamwe
Mageti ya uwanja wa Benjamin Mkapa yamefunguliwa majira ya saa sita mchana tayari kwa mashabiki kuingia uwanjani
Post a Comment