Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Robertinho amesema anatambua mchezo huo hautakuwa mwepesi kwane wanakwenda kuchuana na timu iliyoimarika ambayo imetoa ushindani kwa timu zilizojuu kwenye msimamo wa ligi
"Hautakuwa mchezo rahisi lakini tunahitaji kucheza vizuri na kupata ushindi ili tusonge mbele hatua ya nusu fainali. Tunajua tunakwenda kukutana na timu ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda mchezo huo ili kutimiza malengo yetu," alisema Robertinho
Ihefu Fc tayari iko jijini Dar es salaam kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye ligi katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0
Baada ya mchezo wa kombe la FA, timu hizo zitaelekea Mbarali Mbeya kwa ajili ya mchezo wa duru ya pili ligi kuu ambapo utapigwa April 10 katika uwanja wa Highland Estates
Post a Comment