Katibu mkuu Tff amshangaa Fei Toto - EDUSPORTSTZ

Latest

Katibu mkuu Tff amshangaa Fei Toto

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ Angetile Osiah ameonesha kushangazwa na kinachoendelea kati ya Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’, Young Africans na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF.


Feisal Salum amelitaka Shirikisho la Soka TFF kuvunja mkataba wake na Young Africans baada ya kukwama mara mbili mfululizo mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, ambayo ilikiri kumtambua kama Mchezaji halali wa Young Africans.


Angetille ambaye ni Mwandishi wa Habari za Michezo Mwandamizi nchini Tanzania, ameibuka na andiko alilolichapisha katika Mitandao ya Kijamii akionesha kushangazwa na mvutano, ambao amedai hauna tija zaidi ya Mchezaji kutambua taratibu za kuvunja mkataba, na sio kuihusisha Taasisi ambayo haina uwezo huo.


Angetille ameandika: Mpira wetu unaenda siko. Mchezaji ana mkataba na klabu, halafu anaiomba taasisi nyingine ivunje huo mkataba! Logic inakataa kabisa.


Afadhali angetaja hayo manyanyaso, lakini inaonekana ni utashi tu wa kutaka kuondoka. Huu ni ubabaishaji. Mtu ambaye amechoshwa na ubabaishaji angeomba kuondoka na klabu ambayo inamtaka ingejitokeza kumalizana na muajiri wake.


Football ina kanuni tofauti na ajira nyingine ambazo unaweza kuvunja mkataba wakati wowote unapopata greener pasture. Hivi akivunja mkataba ndio ataanza kutafuta klabu inayomfaa?


Hizo ni sinema, Uaminifu na uadilifu wa mtu hupimwa katika mambo kama haya. Respect aliyoipata na vitu vinavyofanyika ni vitu viwili tofauti. Alishakuwa mchezaji mkubwa lakini anazidi kushusha hadhi yake. Kuaminika baadaye huko aendako itakuwa issue”



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz