Fiston Mayele akitaka kiatu kombe la Shirikisho - EDUSPORTSTZ

Latest

Fiston Mayele akitaka kiatu kombe la Shirikisho

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Huu unaweza kuwa msimu bora zaidi kwa mshambuliaji Fiston Mayele ambaye anawania rekodi ya aina yake katika ligi kuu ya NBC na kombe la Shirikisho barani Afrika


Mayele anaongoza mbio za kuwania ufungaji bora ligi kuu ya NBC akiwa na mabao 16, mabao sita zaidi ya Moses Phiri na Saido Ntibazonkiza wa Simba wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na mabao 10


Aidha katika michuano ya CAF CC, Mayele anaongoza pia akiwa amefunga mabao matano sawa na Ranga Chivaviro wa Malumo Ganants wote wakifunga mabao matano


Mayele ameweka wazi shauku yake ya kuwa mfungaji bora wa ligi na kombe la Shirikisho ili kupamba msimu wake bora zaidi katika maisha yake ya kusakata kabumbu


"Yatakuwa mafanikio makubwa kwangu kama nitafanikiwa kuwa mfungaji bora wa mashindano ya CAF. Nawashukuru wachezaji wenzangu, tunashirikiana vizuri kuhakikisha tunatimiza malengo ya timu, lakini kama itatokea nimekuwa mfungaji bora nitafurahi sana"


"Mwaka jana sikushinda ufungaji bora wa ligi lakini mwaka huu naona inawezekana bado kuna mechi zimebakia, naweza kufanikiwa," alisema Mayele


Msimu huu Mayele amepachika mabao 31 katika michuano yote na kufikisha mabao 50 tangu alipojiunga na Yanga mwaka 2021Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz