Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wamekuwa na muda mzuri wa maandalizi kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa kesho Jumapili
Kaze amebainisha kuwa siku mbili za mazoezi walizopata Lubumbashi zinatosha kuwaweka tayari kwa mchezo huo ambao Yanga inahitaji kushinda
"Tumefanya mazoezi mazuri jana baada ya safari ndefu na pua leo tutapata nafasi ya kujiandaa vizuri na mchezo wa kesho"
"Wachezaji wote wako vizuri naamini tutakuwa na mchezo kesho," alisema Kaze
Akizungumzia kikosi, Kaze amesema wachezaji Djigui Diarra na Khalid Aucho wataukosa mchezo huo wakitumikia adhabu ya kadi tatu za njano
Lakini pia kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki hatakuwa sehemu ya mchezo baada ya kuchelewa kutua DR Congo kutokana na changamoto ya usafiri akitoka kwenye majukumu ya timu ya Taifa
Kocha Mkuu Nasreddine Nabi nae hakusafiri na timu DR Congo kutokana na matatizo ya kifamilia
"Kocha mkuu Nasreddine Nabi ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Mazembe kwa sababu za Kifamilia. Mchezo huu ni muhimu sana kwetu kwa sababu malengo yetu ni kuwa vinara kwenye hatua hii ya Makundi"
No comments:
Post a Comment