Dabi ya Dodoma yasogezwa mbele - EDUSPORTSTZ

Latest

Dabi ya Dodoma yasogezwa mbele

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Dabi ya Dodoma kati ya Fountain Gate Princess dhidi ya Baobab Queens sasa itapigwa Mei 29 kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini hapa ambapo awali ilitakiwa ichezwe Mei 16 mwaka huu.


Msimu uliopita Boabab Queens ilipoteza michezo yote miwili kwa Fountain ikikubali kichapo cha mabao 3-1 mzunguko wa kwanza na mzunguko wa pili wakifungwa bao 1-0 Uwanja wa Fountain Gate Arena.


Baobab Queens msimu huu haina matokeo mazuri kwani katika michezo 14 iliyocheza hadi sasa imepoteza sita, imeshinda mitano na kutoa sare mitatu, ina pointi 18 inashika nafasi ya saba kwenye msimamo.


Fountain msimu huu ni wa moto kwani katika michezo 14 imeshinda 10, imefungwa miwili na kutoa sare miwili, ina pointi 32 inashika nafasi ya tatu huku JKT Queens ikiongoza ikiwa na alama 34.


Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Mkoa wa Dodoma, Tatu Said alisema mabadiliko hayo wameyapokea na maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yanaendelea.


Chanzo: MwanaspotiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz