Bangala atia neno kupangwa na Rivers United - EDUSPORTSTZ

Latest

Bangala atia neno kupangwa na Rivers United

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kiungo wa Yanga, Yannick Bangala amesema hawapaswi kuwadharau wapinzani waliopangwa nao kwenye hatua ya Robo Fanaili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, kwa sababu hatua waliyofikia inathibitisha ubora wao.


Bangala amesema kitu cha msingi kwao ni kutumia muda uliopo kujipanga na kurekebisha mapungufu yao, ambayo yalijitokeza kwenye mechi za hatua ya makundi ili waweze kutimiza malengo yao.


"Nikweli Yanga tuna kikosi bora, lakini huwezi kuwabeza Rivers United ni timu bora na ndio maana imefika hatua hiyo, kitu cha msingi ni kuwaheshimu na kuweka nguvu kwenye maandalizi yetu kabla ya kukutana nao"


"Kwa ushirikiano na umoja wetu tunaweza kufanikiwa, tutawaheshimu kama tulivyofanya kwa timu zote kwenye hatua ya makundi lakini tutaweka mbele malengo yetu" alisema Bangala


Mashabiki wa Yanga wana shauku kubwa kuelekea mchezo dhidi ya Rivers United wakikumbuka matokeo ya msimu uliopita kwenye hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa wakipoteza mechi zote mbili kwa bao 1-0 nyumbani na ugenini


Hata hivyo msimu huu watakutana na Yanga iliyoimarika zaidi ambayo imemaliza makundi ya Shirikisho ikiwa kileleni mwa kundi DDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz