Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kamwe amesema ni kawaida kwa timu yoyote kupitia nyakati za kupoteza mchezo lakini jambo muhimu ni kuhakikisha hawatoki katika malengo yao makuu ambayo ni kushinda makombe
"Tukiwa na Unbeaten 49, Tukapoteza dhidi ya Ihefu, Tena ikiwa kwenye nafasi ya mwisho kwenye msimamo. Ilituumiza. Lakini nini kilifata baada ya pale? Tulishinda mechi 13 za Ligi mfululizo. Tukafuzu Robo Fainali ya CAF. Na kama haitoshi, Tukafuzu Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam"
"Unafikiri hayo yote yalitokea kwa bahati mbaya? Si kweli. Siri nyuma yake ni Kutopoteza malengo. MALENGO yetu ni Nini msimu huu? kubeba makombe. Kila Mwanayanga anataka kuiona Timu yake ikibeba Kombe la Ligi, Kombe la Shirikisho la Azam na Ubingwa wa Afrika"
"Tunaimaliza April. Mwezi unaofata, utakuwa mwezi wa mapigano makubwa katika kuyafikia malengo yetu. Vyakula vyote vizuri bado viko juu ya meza yetu. Tutulie na Tushikane Wananchi"
"Kupoteza pambano sio kupoteza vita. Jana Tumepoteza pointi 3, hatujapoteza Malengo yetu ya Ubingwa Msimu huu," aliandika Kamwe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii"
Licha ya kipigo kutoka kwa watani zao Simba hapo jana, Yanga imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi ya NBC ikiwa na alama 68 huku Simba ikipunguza gap la pointi kutoka nane na kubaki tano baada ya kufikisha alama 63
Kila timu imesalia na mechi nne kuhitimisha msimu Yanga ikihitaji alama nane kutetea ubingwa
Post a Comment