Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Yanga imetinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya US Monastir
Mabao ya Kennedy Musonda na Fiston Mayele yameihakikishia Yanga alama tatu muhimu ambazo sio tu zimewapeleka Wananchi robo fainali ya kombe la Shirikisho, Wananchi wamekaa kileleni mwa kundi D wakiwa na uwiano mzuri wa mabao kuliko Monastir
Ilikuwa mechi ambayo awali ilionekana kama ingekuwa ngumu kutokana na mazingira ya mvua kubwa kunyesha kwa saa kadhaa kabla ya mchezo
Hata hivyo wachezaji wa Yanga walipambana kuhakikisha wanautendea haki uwanja wa nyumbani na kuibuka na ushindi huo muhimu
Yanga imefikisha alama 10 ikiwa vinara wa kundi D sawa na Monastir
TP Mazembe wamepoteza mchezo dhidi ya Real Bamako kwa kuchapwa mabao 2-1 na hivyo kushushwa nafasi ya nne
Real Bamako wamepanda nafasi ya tatu wakiwa alama 5
No comments:
Post a Comment