Jana Arsenal ililazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Sporting katika mchezo wa 16 bora ligi ya Europa
Pamoja na kucheza vizuri, Arsenal walionekana kuwa na changamoto kwenye eneo la umaliziaji. Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta alibainisha kuwa kukosekana kwa baadhi ya washambuliaji wake ilikuwa changamoto
Arteta alieleza kuridhika na matokeo hayo ya ugenini akiamini timu yake inaweza kufanya vizuri zaidi katika mchezo watakaocheza nyumbani
Pamoja na kurejea mazoezini wiki hii, mshambuliaji Gabriel Jesus bado hajapata nafasi ya kuitumikia Arsenal
Wengi walitamani kumuona Jesus kwenye kikosi kwa ajili ya mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Europa baada ya mshambuliaji huyo kurejea mazoezini lakini Arteta hana haraka akiamini bado kuna mechi za kutosha kwa ajili yake kuisaidia timu hiyo
Gabriel Martinelli alianza eneo la ushambuliaji wakati Jesus na Eddie Nketiah wakikosekana
Leandro Trossard pia alikosekana na hivyo Emile Smith Rowe kuwa mshambuliaji aliyebaki eneo la akiba
Arsenal walimiliki mpira muda mwingi ingawa Sporting walitengeneza nafasi za wazi zaidi
No comments:
Post a Comment