Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Bayern Munich wameamua kumfukuza meneja Julian Nagelsmann, 35, huku Mjerumani mwenzake na meneja wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel akiwa mgombea anayeongoza kuchukua nafasi yake. (Bild – In Germany)
Tottenham inaweza kumgeukia Nagelsmann kama mbadala wa Muitaliano Antonio Conte, 53, ambaye anaonekana kutaka kuondoka katika klabu hiyo ya Ligi ya Premia. (Soccer.London)
Chelsea, Manchester City na Newcastle United wanafikiria kumnunua winga wa Juventus Mwingereza mwenye umri wa miaka 19 Samuel Iling-Junior msimu wa joto. (90 min)
Mshambulizi wa Uingereza Marcus Rashford, 25, atasita kusaini mkataba mpya na Manchester United hadi wamiliki wapya wa klabu hiyo watakapothibitishwa. (Sun)
Arsenal wameungana na Leeds, AC Milan na Sevilla katika mbio za kuwania saini ya Mchezaji wa Kimataifa wa U-19 wa Barcelona na Uhispania Ilias Akhomach, 18. (Sport - in Spanish)
Liverpool wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester United kupata huduma za gwiji wa kuajiri Paul Mitchell, 41, ambaye ataondoka Monaco msimu huu wa joto. (Mirror)
Manchester City wanafanyia kazi mpango wa kumnunua beki wa kati wa Hajduk Split Luka Vuskovic lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Paris St-Germain kumnunua Mkroatia huyo mwenye umri wa miaka 16. (Fabrizio Romano)
Everton wamejiunga na Newcastle katika kufikiria kumnunua mshambuliaji wa Brazil Giovani, 19, anayechezea Palmeiras. (ESPN Brazil – In Portugal)
Everton itamnunua mshambuliaji wa Ufaransa Neal Maupay, 26, kwa ajili ya kuuzwa msimu wa joto. (Football Insider) Nafasi ya fowadi wa Argentina Lionel Messi, 35, kuondoka Paris St-Germain na kujiunga na klabu yake ya zamani ya Barcelona inaongezeka. (90min)
Barcelona huenda ikafungiwa kucheza soka la Ulaya msimu ujao baada ya Uefa kuanzisha uchunguzi kuhusu malipo yaliyotolewa kwa aliyekuwa makamu wa rais wa kamati ya waamuzi ya Uhispania. (Sun)
Beki wa Manchester United na Uswidi Victor Lindelof, 28, atafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake mwishoni mwa msimu huu. (Mirror)
Wasiwasi unaongezeka miongoni mwa baadhi ya vyama vinavyotaka kuinunua Manchester United kwamba familia ya Glazer inaweza kuchagua kutoiuza klabu hiyo. (Guardian)
BBC
Post a Comment