Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Real Madrid wanafuatilia yanayoendelea na mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 29, ambaye mkataba wake unamalizika 2024 na amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kuhamia Manchester United au Bayern Munich. (Mail)
Kipengele cha kuachiwa cha euro 200m (£175m) kilichoandikwa katika kandarasi ya Erling Haaland na Manchester City si halali tena na klabu itaweza kuweka bei yao wenyewe iwapo itataka kumuuza mshambuliaji huyo wa Norway, 22, ambaye yuko chini ya kandarasi hadi 2027. (Goal)
Brighton wako tayari kumpa winga wa Kijapani Kaoru Mitoma, 25, mkataba utakaoweka rekodi huku Real Madrid, Manchester City na Arsenal wakionesha nia yao. (Goal)
Patrick Vieira alitimuliwa kama meneja wa Crystal Palace kwa sababu iliaminika alikuwa mpole sana kwa wachezaji wake ambao hawakucheza vizuri. (Mirror)
Chelsea ina "nia na shauku ya juu" kumsajili mchezaji wa West Ham Declan Rice, 24, msimu ujao - kiungo huyo wa kati wa safu ya ulinzi wa Uingereza ana mkataba Uwanja wa London hadi 2024. (Florian Plettenberg)
Kiungo wa kati wa Ufaransa anayesumbuliwa na majeraha N'Golo Kante, 31. - ambaye hajacheza tangu Agosti kwa sababu ya tatizo la misuli ya paja lakini anaendelea kurejea katika hali nzuri - "yuko tayari" kusaini mkataba mpya wa miaka miwili Chelsea. (Sun)
Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, ambaye amekuwa akilengwa kwa muda mrefu na Manchester United na Chelsea, alisema katika mahojiano kwenye televisheni ya Uhispania: "Barca imekuwa klabu ya ndoto zangu siku zote... natumai kuendelea huko kwa miaka mengine mengi". (TV3 - in Catalan)
Kiungo wa kati wa Nigeria Alex Iwobi, 26, ambaye mkataba wake wa sasa na Everton unaendelea hadi msimu wa 2024, amepewa mkataba mpya lakini anasubiri kuona jinsi msimu utakavyoisha kabla ya kuusaini. (Football Insider)
Liverpool itawaruhusu kiungo wa kati wa zamani wa England Alex Oxlade-Chamberlain, 29, na Naby Keita, 28, wa Guinea kuondoka kama wachezaji huru msimu ujao, huku Mbrazil Arthur Melo, 26, akirejea Juventus mwishoni mwa mkataba wake wa mkopo huku Jurgen Klopp akiomba kujenga upya safu yake ya kiungo wa kati. (Athletic - subscription required)
Kiungo wa kati wa Bayern Munich na Uholanzi Ryan Gravenberch, 20, amekamilisha uhamisho wa kwenda Liverpool, kulingana na mchezaji wa zamani wa Reds Jose Enrique, ambaye alifichua hayo kwenye mtandao, moja kwa moja. (Sun)
Winga wa Napoli wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 22, ambaye amekuwa akihusishwa na Real Madrid na Manchester City, anaweza kushawishika kujiunga na Newcastle ikiwa watafuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao. (Football Insider)
Barcelona itakuwa tayari kuwauza viungo Ousmane Dembele, 25, wa Ufaransa, na Ferran Torres, 23, wa Uhispania, ili kupata pesa za kufadhili usajili wa mshambuliaji wa Juventus wa Italia Federico Chiesa, 25. (Calciomercato - in Italian)
Kiungo wa kati wa zamani wa Uhispania Sergio Busquets, 34, amepewa ofa ya kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja na Barcelona, kukiwa na chaguo la mwaka mmoja zaidi, lakini pia anaangalia uwezekano wa kuhamia Inter Miami au Toronto kwenye MLS, na amepewa ofa kutoka vilabu vitatu nchini Saudi Arabia. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Manchester United wamepanga kumteua mtendaji mkuu wa Adidas Matt Hargreaves, ambaye ana historia ya sheria na ni shabiki wa United, kuongoza mazungumzo yao ya uhamisho wa soka. (Athletic - subscription required)
BBC
No comments:
Post a Comment